VOOZH about

URL: https://www.trtafrika.com/swahili/article/718ceb42bc45

⇱ Mlipuko mwingine wa kipindupindu waripotiwa Burundi - TRT Afrika


| Swahili
| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mlipuko mwingine wa kipindupindu waripotiwa Burundi
Kulingana na waziri wa afya wa nchi hiyo, kwa sasa, jumla ya wagonjwa 34 wanapatiwa matibabu katika vituo mbalimbali vya afya.
πŸ‘ Mlipuko mwingine wa kipindupindu waripotiwa Burundi
Kulingana na Barahadana, wagonjwa wapya walikuwa wakipokea matibabu katika vituo mbalimbali vya afya./Picha:@MSF

Serikali ya Burundi imetangaza mlipuko mwingine wa ugonjwa kipindupindu nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Lydwine Baradahana alisema ya jitihada za kuudhibiti ugonjwa huo, bado hali si ya kuridishisha kwani kuna jumla ya wagonjwa 34 wanaopokea matibabu.

 β€œHii ni mara ya kwanza kwa mwaka kukutana na hali kama hii,” alisema waziri huyo.

Kulingana na Barahadana, wagonjwa wapya walikuwa wakipokea matibabu katika vituo mbalimbali vya afya, ikiwemo hospitali ya Prince Regent Charles.

ZILIZOPENDEKEZWA
ZILIZOPENDEKEZWA

Alitadhaharisha kuhusu uchafu wa mazingira, akisema kuwa ndiyo sababu kubwa iliyopelekea maambukizi hayo mapya.

Serikali ya Burundi ilitenga Dola milioni 1 katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.

Kulingana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), mataifa 23 yalikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu mwaka jana.

ZILIZOPENDEKEZWA
ZILIZOPENDEKEZWA
Soma zaidi