Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan, alisema Jumatano kuwa mashambulizi ya Israel nchini Syria na Lebanon yamefikia kiwango ambacho sasa yanaihatarisha pia Uturuki. Aliongeza kuwa βuchokoziβ wa Israel ni tishio kwa dunia nzima na lazima ukomeshwe.
Akilihutubia Bunge la Taifa, Erdogan aliishutumu Israel kwa kuchukua hatua ambazo zinaweza kuongeza ukosefu wa utulivu katika eneo la Mashariki ya Mediterania na kanda nzima.
βUsalama wa Uturuki hauanzi Hatay pekee, bali pia Aleppo, Damascus na Beirut. Hatuwezi kukubali hali yoyote ya kutumia nguvu katika nchi za ndugu zetu, wala hatutafumbia macho uchokozi,β alisema, akisisitiza kuwa usalama wa nchi yake unaenea zaidi ya mipaka yake.
Rais Erdogan pia aliashiria kile alichokiita βdhana potofu ya Ardhi ya Ahadiβ ya Waisraeli, akisema kuwa Uturuki inaelewa kikamilifu lengo lao la mwisho.
βKwa mapenzi ya Mungu, hatutaruhusu jambo hilo kamwe,β alisema.
Akiyaonya mataifa dhidi ya kujiweka upande wa Israel, Erdogan alisema: βHakuna anayepaswa kutafuta hatari au kujiingiza katika majaribio yasiyo na busara. Hakuna anayepaswa kufuata mkondo wa mtandao wa mauaji wa Kizayuni.β
βIsrael lazima izuiweβ
Kiongozi huyo wa Uturuki alionya kuwa kushindwa kuzuia hatua za Israel kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa kanda na kwa jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.
βIkiwa uharamia wa Israel hautakomeshwa, dunia nzima pamoja na eneo hili itabeba matokeo yake,β alisema.
βIsraeli lazima izuiwe. Hili ni jukumu la ubinadamu ... historia haipaswi kuruhusiwa kujirudia.β
Erdogan pia alionya kwamba Uturuki itajibu kwa nguvu hatua yoyote itakayolenga haki za raia wa Uturuki au za Kupro ya Kituruki katika eneo la Mashariki ya Mediterania.
βIkiwa haki za Uturuki na za Waturuki wa Kupro katika Mashariki ya Mediterania zitaguswa au kulengwa, nataka ijulikane kwamba majibu yetu yatakuwa wazi kabisa na makali sana,β alisema Erdogan.
